David Miliband: Mgogoro wa wakimbizi ni kipimo cha utu wetu

TED2017

David Miliband: Mgogoro wa wakimbizi ni kipimo cha utu wetu


Watu millioni sitini na tano walitolewa katika makazi yao na migogoro na majanga katika mwaka 2016. Huu sio tu ni mgogoro; lakini pia ni kipimo cha kuwa sisi ni nani na tunasimamia nini, anasema David Miliband - kila moja wetu ana jukumu binafsi kutatua hali hii. Katika mazungumzo haya yenye umuhimu wa kipekee kuyaangalia , Miliband anatupa njia za dhahiri za kuwasaidia wakimbizi na kugeuza huruma na kuwawazia wengine kuwa vitendo.

Anne Lamott: Ukweli 12 niliojifunza kupitia maisha na uandishi

TED2017

Anne Lamott: Ukweli 12 niliojifunza kupitia maisha na uandishi


Siku chache kabla ya kutimiza miaka 61, mwandishi Anne Lamott aliamua kuandika kuhusu kila kitu alichofahamu kwa hakika. Anazama katika mihangaiko ya mwanadamu anayeishi katika ulimwengu uliochanganika, wenye uzuri na hisia, unaompa hekima na ucheshi kuhusu familia, uandishi, maana ya Mungu, kifo na zaidi.

Sofi Tukker: "Awoo"

TEDNYC

Sofi Tukker: "Awoo"


Kundi la wanamuziki wawili wa Electro-pop linalofahamika kama Sofi Tukker likicheza na umati wa TED katika nyimbo yao ya mdundo wa haraka ya "Awoo", wakimshirikisha Betta Lemme.

Sitawa Wafula: Kwanini naongelea kuhusu kuishi na kifafa

TEDNairobi Ideas Search

Sitawa Wafula: Kwanini naongelea kuhusu kuishi na kifafa


Aliyewahi kubaki nyumbani kutokana na ugonjwa wa kifafa. Sitawa Wafula, ambae ni mhamasishaji wa afya ya akili alipata nguvu kuandika kuhusu ugonjwa wake. Kwa sasa, anahamasisha kwa ajili ya wengine ambao bado hawajatambua sauti zao, akivunja unyanyapaa na kutengwa katika kuongelea ni namna gani inavyokuwa kwa mtu anayeishi na ugonjwa wa kifafa.

Karim Abouelnaga: Shule ya kiangazi watakayo watoto

TED2017

Karim Abouelnaga: Shule ya kiangazi watakayo watoto


Kipindi cha kiangazi, watoto toka kaya maskini Marekani husahau karibu miezi mitatu ya walichosoma kipindi cha mwaka wa shule. Mjasiriamali wa elimu na Mshirika wa TED Karim Abouelnaga anataka kurekebisha upotevu huu wa elimu, kwa kubadili "anguko la kiangazi" kuwa fursa ya kwenda mbele na kukua kuelekea baadaye ing'arayo zaidi.

Stephanie Busari: Jinsi gani habari za uongo huleta madhara ya kweli

TEDLagos Ideas Search

Stephanie Busari: Jinsi gani habari za uongo huleta madhara ya kweli


Mnamo Aprili 14, 2014, shirika la kigaidi la Boko Haram liliteka zaidi ya wasichana wa shule 200 kutoka mji wa Chibok, Naijeria. Duniani kote, uhalifu huu ulifanywa mfano kwa kauli mbiu ya #BringBackOurGirls yaani "Rejesha Wasichana Wetu" -- lakini ndani ya Naijeria, maafisa wa serikali waliita uhalifu huu kuwa ni mzaha, kusababisha utata na kuchelewesha jitihada zozote za kuwakomboa wasichana hawa. Katika zungumzo hili shupavu, mwanahabari Stephanie Busari anaelekezea janga la Chibok kueleza hatari kubwa ya habari za uongo na nini tunaweza kufanya kuzizuia.

Todd Scott: Mwongozo wa Kifalaki wa kutumia difibrileta

TEDNYC

Todd Scott: Mwongozo wa Kifalaki wa kutumia difibrileta


Ikiwa Yoda atapata mshtuko wa moyo, utajua nini cha kufanya? Msanii na mkereketwa wa Huduma ya Kwanza Todd Scott anachambua kila kitu unachotakiwa kufahamu kuhusu kutumia AED, "Automated External Defibrillator", kwenye falaki hii na nyingine za mbali. Jiandae kuokoa maisha ya Jedi, Chewbacca (atahitaji kunyolewa kidogo kwanza) au mwingine yeyeote mwenye kuhitaji pamoja na dondoo zenye msaada. AED ni kifaa-tiba kinachotumia umeme kurudisha mapigo ya moyo katika mwendo wa kawaida

Sara Ramirez: "Rollercoaster" (Gari-bembea)

TED Talks Live

Sara Ramirez: "Rollercoaster" (Gari-bembea)


Mwimbaji, mwandishi wa nyimbo na mwigizaji Sara Ramirez ni mwanamke mwenye vipaji vingi. Akiungana na Michael Pemberton kwenye gitaa, Ramireza anaimba juu ya fursa, hekima na kuinuka na kuporomoka kwenye maisha katika tamasha hili mubashara la wimbo wake, "Rollercoaster." Rollercoaster ni bembea mfano wa gari moshi ambayo reli yake inapanda juu sana na kushuka chini. Watu husikia raha wakati wa kupanda au ikiwa juu lakini huogofya wakati wa kushuka chini, kwani huwa kama yaanguka. Carousel ni bembea mfano wa farasi wanaokwenda wakizunguka duara. Farasi (au viti mfano wa kitu chochote) hufungwa kwenye kamba ipandayo na kushuka mithili ya mwendo wa farasi huku ikizunguka mduara.

Thordis Elva, Tom Stranger: Simulizi letu la ubakaji na maridhiano

TEDWomen 2016

Thordis Elva, Tom Stranger: Simulizi letu la ubakaji na maridhiano


Mwaka 1996, Elva Thordis alifurahia penzi la utotoni na Tom Stranger, mwanafunzi kutoka Australia. Baada ya sherehe ya Krismasi shuleni, Tom alimbaka Thordis, nahawakukutani baada ya miaka mingi. Katika majadiliano hayo ya ajabu, Elva na Stranger wanazungumzia miaka ya kuishi katika aibu na usiri, na kutualika kujadili changamoto ya hii kimataifa juu ya unyanyasaji wa kijinsia katika uaminifu mpya. Kwa mjadala, tembelea go.ted.com/thordisandtom.

Charity Wayua: Njia chache za kurekebisha Serikali

TED@IBM

Charity Wayua: Njia chache za kurekebisha Serikali


Charity Wayua aliweka ujuzi wake kama mtafiti wa kansa kwa mgonjwa asiyetarajiwa: Serikali ya nchi yake ya Kenya. Anaeleza jinsi yeye alisaidia serikali yake kwa kiasi kikubwa kuboresha mchakato wake kwa ajili ya kufungua biashara mpya, sehemu muhimu ya afya ya kiuchumi na ukuaji, na hivyo kusababisha miradi mipya na kutambuliwa na Benki ya Dunia kama mboreshaji mkuu.

Adam Grant: Je, wewe ni mtoaji au mpokeaji?

TED@IBM

Adam Grant: Je, wewe ni mtoaji au mpokeaji?


Katika kila mahali pa kazi, kuna aina tatu za msingi za watu: watoaji, wapokeaji na walipizaji. Mwanasaikoloji Adam Grant anazifafanua hizi nafsi tatu na anatoa mikakati ya kukuza utamaduni wa ukarimu na jinsi ya kuwaepuka wafanyakazi wabinafsi kuchukua zaidi kuliko sehemu yao.

Chinaka Hodge: Utawaambia mabinti wako nini kuhusu mwaka 2016?

TEDWomen 2016

Chinaka Hodge: Utawaambia mabinti wako nini kuhusu mwaka 2016?


Kwa maneno makali kama vipande vya glasi, Chinaka Hodge anaukata wazi mwaka 2016, na kuwacha miezi 12 za vurugu, huzuni, hofu, aibu, ujasiri na matumaini ya mwagike nje katika shairi hili la kiasili kuhusu mwaka ambao hamna kati yetu atausahau

Rebecca MacKinnon: Tunaweza kupambana na ugaidi bila kutoa kafara haki zetu

TEDSummit

Rebecca MacKinnon: Tunaweza kupambana na ugaidi bila kutoa kafara haki zetu


Tunaweza kupambana na ugaidi bila kuharibu demokrasia? Mwanaharakati wa Uhuru wa mtandao wa intaneti Rebecca MacKinnon anafikiri kwamba tutashindwa kwenye vita hii dhidi ya siasa kali na siasa za fujo ikiwa tutadhibiti mtandao wa intaneti na vyombo vya habari. Katika mazungumzo haya muhimu ametoa wito wa kusimama kidete kuhusu taarifa zilizodhibitiwa usiri na kuzitaka serikali kutumia njia bora kulinda, na sio kunyamazisha, waandishi wa habari na wanaharakati wanaopambana dhidi ya wenye siasa kali.

Ngozi Okonjo-Iweala: Jinsi gani Afrika itaendelea kukua

TEDSummit

Ngozi Okonjo-Iweala: Jinsi gani Afrika itaendelea kukua


Ukuaji wa Kiafrika ni harakati, sio ubabaishaji, anasema mchumi na aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala. Katika mazungumzo haya ya kusisimua yaliyo wazi,Okonjo Iweala anaelezea hatua endelevu barani na kuainia changamoto nane ambazo mataifa ya Kiafrika bado yanahitaji kuzungumzia ili kuweza kuwa na maisha bora baadaye.

Kang Lee: Unaweza kujua kweli kama mtoto anadanganya?

TED2016

Kang Lee: Unaweza kujua kweli kama mtoto anadanganya?


Je watoto hawadanganyi vizuri? Unafikiri unaweza kugundua uwongo wao kwa urahisi? Mtafiti wa maendeleo Kang Lee amechunguza nini kinatokea kisaikolojia kwa watoto wanapodanganya. Wanafanya mara nyingi kuanzia umri mdogo wa miaka miwili, na hakika wanafanya vizuri kweli. Lee anaelezea kwanini tusherehekee wakati watoto wanaanza kudanganya na kuwasilisha teknolojia mpya ya kugundua uwongo ambayo siku moja itaonyesha hisia zetu zilizojificha.

Jennifer Kahn: Ubadilishwaji wa Jeni sasa unaweza kubadili spishi nzima- milele

TED2016

Jennifer Kahn: Ubadilishwaji wa Jeni sasa unaweza kubadili spishi nzima- milele


Ubadilishaji jeni wa CRISPR unaruhusu wanasayansi kubadilisha mfumo wa DNA na kuthibitisha kwamba matokeo ya ubainishaji kijenetiki uliorekebishwa unarithiwa na vizazi vijavyo, na kufungua uwezekano wa kurekebisha spishi milele. Zaidi ya kitu chochote, teknolojia imepelekea maswali: Jinsi gani nguvu hii mpya itaathiri ubinadamu? Tutaitumia kubadilisha nini? Tumekuwa miungu sasa? Jiunge na mwandishi wa habari Jennifer Kahn anayejiuliza maswali haya na kuelezea ubadilishaji jeni: kutengenezwa kwa mbu wanaokinzana na magonjwa ambao wanaweza kutokomeza malaria na Zika.

Aditi Gupta: Njia isiyo na mwiko kuongelea kuhusu siku za hedhi

TEDxGatewayWomen

Aditi Gupta: Njia isiyo na mwiko kuongelea kuhusu siku za hedhi


Ni kweli: kuongelea kuhusu hedhi kunafanya watu wengi wakose raha. Na mwiko huo una matokeo yake: nchini India, wasichana watatu kati ya 10 hawajui hata hedhi ni nini wakati wa siku zao za kwanza, na masharti ya mila yanayohusiana na siku za hedhi yanaleta uharibifu kisaikolojia kwa wasichana. Kukua katika mwiko huu mwenyewe, Aditi Gupta alijua anataka kusaidia wasichana, wazazi, waalimu kuzungumzia kuhusu siku za hedhi kwa raha bila aibu. Anatushirikisha alivyofanya.

Alaa Murabit: Je dini yangu inasema nini hasa kuhusu wanawake?

TEDWomen 2015

Alaa Murabit: Je dini yangu inasema nini hasa kuhusu wanawake?


Familia ya Alaa Murabit ilihamia Canada kutoka Libya alipokuwa na miaka 15. Kabala alijiona yuko sawa na kaka zake, lakini katika mazingira haya mapya alihisi vizuizi kuhusu yale mafanikio anayoweza kuyapata. Kama mwanamke wa Kiislam , alijiuliza kama haya kweli ni mafundisho ya dini? Kwa namna ya kuchangamsha anatushirikisha ugunduzi wa mifano ya viongozi wanawake katika historia ya imani yake - Na jinsi alivyoanzisha kampeni ya kupigania haki za wanawake kwa kutumia mistari ya Korani.

Memory Banda: Kilio cha shujaa dhidi ya ndoa za utotoni

TEDWomen 2015

Memory Banda: Kilio cha shujaa dhidi ya ndoa za utotoni


Maisha ya Memory Banda yalichukua njia ya tofauti na maisha ya dada yake. Dada yake alipovunja ungo, alipelekwa katika kambi ya awali ambayo inafundisha wasichana "jinsi ya kumridhisha mwanaume kimapenzi" Akapata uja uzito huko - akiwa na umri wa miaka 11. Lakini Banda akakataa kwenda. Badala yake , akaandaa wengine na akamuomba kiongozi wa jamii yake kupitisha sheria ndogo inayozuia wasichana kulazimishwa kuolewa kabla ya kufikisha miaka 18. Akaendeleza mapambano haya mpaka katika ngazi ya kitaifa ... akipata matokeo ya ajabu sana kwa wasichana wote , katika nchi yote ya Malawi.

Boniface Mwangi: Siku niliposimama peke yangu

TEDGlobal 2014

Boniface Mwangi: Siku niliposimama peke yangu


Mnasa picha Boniface Mwangi alitaka kupinga ufisadi nchini mwake Kenya. Hivyo aliweka mpango. Yeye na marafikize wangesimama na kupiga makelele kwenye mkutano wa hadhara. Lakini wakati huo ulipowadia…alisimama peke yake. Kilichotokea baadaye, anasimulia, kilimdhiririshia alikuwa mtu wa aina gani. Anavyosema, “Kuna siku mbili za umuhimu mkuu maishani mwako. Siku ya kuzaliwa, na siku utakavyogundua kwa nini." Picha za kuogofya.

Ziyah Gafic: Vitu tutumiavyo kila siku, historia ya kusikitisha

TED2014

Ziyah Gafic: Vitu tutumiavyo kila siku, historia ya kusikitisha


Ziyah Gafic anapiga picha vitu tunavyotumia kila siku-saa, viatu, miwani. Lakini vitu hivi vinaonekana ni vya kawaida; vilifukuliwa kutoka katika makaburi ya watu waliokufa kutokana na vita ya Bosnia. Gafic, ambaye ni mshiriki wa TED na mkazi wa Sarajevo, amepiga picha kila kitu kilichotoka katika makaburi yale na kisha kutengeneza maktaba ya kudumu ya utambulisho wa watu waliofariki katika vita hivyo.

Clint Smith: The danger of silence

TED@NYC

Clint Smith: The danger of silence


"We spend so much time listening to the things people are saying that we rarely pay attention to the things they don't," says poet and teacher Clint Smith. A short, powerful piece from the heart, about finding the courage to speak up against ignorance and injustice.

Shai Reshef: Shahada ya gharama nafuu kabisa

TED2014

Shai Reshef: Shahada ya gharama nafuu kabisa


Katika chuo cha mtandaoni cha watu, yeyote aliyemaliza masomo ya sekondari anaweza akasoma masomo ya shahada ya usimamizi wa biashara au sayansi ya kompyuta - bila gharama za kawaida za ada (inagawa mitihani ina gharama zake). Mwanzilishi wake Shai Reshef anatumaini kuwa elimu ya juu inabadilika "kutoka kuwa upendeleo kwa wachache mpaka kuwa haki ya msingi , ambayo inapatikana kwa urahisi na unafuu."

Will Potter: Mpango wa Kustua wa kufanya maandamano na upinzani wa amani kuwa kosa la jinai.

TED2014

Will Potter: Mpango wa Kustua wa kufanya maandamano na upinzani wa amani kuwa kosa la jinai.


Mwaka 2002, Mwandishi wa habari za uchunguzi na TED Fellow Will Potter aliamua kupumzika kazi yake ya mara kwa mara ya kuandika kuhusu mauaji kwa ajili ya gazeti la Chicago Tribune. Alienda kulisaidia kundi linalofanya kampeni kinyume na matumizi ya wanyama katika majaribio ya kisayansi. "Nilifikiri itakuwa ni njia salama ya kufanya jambo jema," anasema . Lakini kinyume chake ,alikamatwa, na hapo ikaanza safari yake kwenye dunia ambayo maandamano ya amani yanaitwa ugaidi.

Ni kitu gani kinahitajika ili kuwa kiongozi bora

TED@BCG San Francisco

Ni kitu gani kinahitajika ili kuwa kiongozi bora


Kuna programu nyingi za uongozi siku hizi, kutoka mafunzo ya siku moja hadi katika mafunzo kwa ajili ya makampuni ya biashara. Kiukweli,hii haitasaidia. Katika hotuba hii ambayo ni makini na halisi ,Bibi Roselinde Torres anaeleza miaka yake 25 ya kuangalia na kutafuta viongozi bora makazini,na anashirikiana nasi haya maswali matatu muhimu ya viongozi wa makampuni kujiuliza ili kuweza kukua na kupata mafanikio.

Stephen Cave: Hadithi nne tunazoambia nafsi zetu kuhusu kifo

TEDxBratislava

Stephen Cave: Hadithi nne tunazoambia nafsi zetu kuhusu kifo


Mwanaphilosophia Steven Cave anaanza kwa swali lenye kazi lakini la kulazimisha kufikiria:Lini ulitambua utakuja kufa?Na cha kusisimua zaidi:Kwa nini wanadamu huwa tunakwepa kifo?Katika hotuba hii ya kuvutia Bwana Cave anachambua vitu vinne katika maisha ya binadamu ambapo huwa tunaambia nafsi zetu "ili kutusaidia kupambana na uoga wa kifo"

David Steindl-Rast: Unataka kuwa na furaha? Kuwa mtu wa Shukrani

TEDGlobal 2013

David Steindl-Rast: Unataka kuwa na furaha? Kuwa mtu wa Shukrani


Kitu kimoja ambacho binadamu wote tunacho pamoja ni kuwa na furaha,anasema kaka David Steindl-Rast,mtawa na mwanafunzi wa imani.Na furaha,anasema,inazaliwa kutoka katika shukrani.Somo linalohamasisha katika kwenda polepole,kuangalia unapokwenda,na kwa hayo yote,kuwa na shukrani.

Robin Nagle: Nilichokigundua katika uchafu wa Jiji la New York

TEDCity2.0

Robin Nagle: Nilichokigundua katika uchafu wa Jiji la New York


Wakazi wa Jiji la New York, wanatengeneza tani 11,000 za uchafu kila siku.Kila Siku! Takwimu hii ya ajabu ni moja ya sababu iliyomfanya Robin Nagle kufanya utafiti pamoja na idara ya usafi.Alipita njia zao,akaendesha mifagio ya umeme, na hata kuendesha gari la taka yeye mwenyewe- yote haya ili aweze kujibu swali linaloonekana kuwa rahisi lakini gumu: Ni nani anayetakiwa kusafisha baada yetu?

Sonia Shah: Sababu tatu kwa nini hatujaitokomeza  malaria

TEDGlobal 2013

Sonia Shah: Sababu tatu kwa nini hatujaitokomeza malaria


Tumejua jinsi ya kutibu malaria tangu 1600,kwanini ugonjwa huu bado unaua maelfu ya mamia kila mwaka?ni zaidi ya tatizo la kitabibu,anasema mwandishi wa habari Sonia Shah.Mtazamo wa historia ya malaria unaweka wazi sababu tatu kwanini ni ngumu kutokomeza malaria

Peter van Manen: Jinsi mbio za magari zinavyoweza kuwasaidia watoto wachanga?

TEDxNijmegen

Peter van Manen: Jinsi mbio za magari zinavyoweza kuwasaidia watoto wachanga?


Wakati wa mbio za magari za Formula 1, gari linatuma mamia ya mamilioni ya taarifa mbalimbali karakana yake kwa ajili ya uchunguzi na upashanaji taarifa kwa wakati huo huo. Kwa hiyo kwa nini tusitumie mfumo huu wa taarifa sehemu nyingine, kama ... katika hospitali za watoto? Peter Van Manen anatueleza zaidi