TEDGlobal 2017
Niti Bhan: Fursa zilizofichwa katika sekta isiyo rasmi
Niti Bhan anatafiti mikakati ya kibiashara kwa soko lisilo rasmi la Afrika: maduka madogo, wabunifu walio na ujuzi na wafanya kazi ambao ni injini isiyoonekana ambayo inafanya uchumi wa bara kusonga mbele. Inashawishi kuwaza kwamba wafanya kazi hawa ni wakwepa kodi, wahalifu -- lakini anaelezea suala hili kwamba kipande hiki ambacho kinakuza uchumi ni halali kinafaa kuwekeza. Kama tutafanya, anasema, tutatengeneza maelfu ya ajira. "Hizi ni mbegu zenye rutuba za biashara na viwanda," Bhan anasema. "Je, tunaweza kuanza kwa kutambua ujuzi huu na kazi?"