TED2019
Muthoni Drummer Queen: Muthoni Malkia wa ngoma akiongea katika TED2019
Muthoni Malkia wa ngoma akiongea katika TED2019
TED2019
Muthoni Malkia wa ngoma akiongea katika TED2019
TED Residency
Mkulima wa kawaida nchini Marekani anapata chini ya senti 15 kwa kila dola moja ya bidhaa utakayonunua katika maduka makubwa. Wanalisha jamii zetu, lakini mara nyingi wakulima hawawezi kumudu chakula kile kile walimacho. katika mazungumzo haya, mjasiriamali wa kijamii Mohammad Modarres anaonyesha jinsi ya kuifanya nguvu yako ya manunuzi ili kuokoa kilimo cha eneo husika kisianguke na kuubadilisha mfumo wa chakula kutoka chini kwenda juu.
TEDxTaipei
Kusoma na kuandika vinaweza kuwa vitendo vya ujasiri vinavyotuleta karibu na watu wengine na karibu na nafsi zetu pia. Mwandishi Michelle Kuo anashirikisha namna ambavyo kufundisha stadi za kusoma kwa wanafunzi wake kule Mississippi Delta kulivyofunua nguvu ya daraja la maneno yaliyoandikwa-- pamoja na mipaka ya nguvu hiyo.
TED2019
Jamii za zamani zilihamishaje mawe makubwa kujenga Stonehenge, mapiramidi na sanamu za Kisiwa cha Easter? Katika mazungumzo haya mafupi , TED Fellow Brandon Clifford, anafumbua siri za zamani na kuonyesha jinsi tunavyoweza kutumia njia hizi kujenga kwa ajili ya siku za baadaye. "Katika zama ambazo tunasanifu majengo kudumu kwa miaka 30, au labda 60," he says, " ningependa kujifunza jinsi ya kutengeneza kitu kitachoburudisha milele."
TED2019
Njia ya uzalishaji nyama ya kawaida inaathiri mazingira yetu na ni athari kwa afya ya ulimwengu, lakini watu hawaendi kupunguza ulaji nyama hadi tuwape chaguo mbadala yanye bei sawia (au ya chini) na ladha sawia (au bora). Kwa hotuba ya kufungua macho, mvumbuzi wa vyakula na mwana TED Bruce Friedrich anaonyesha bidhaa za mimea na chembe ambazo zinaweza kubadilisha sekta ya nyama duniani -- na sahani yako ya chajio.
TEDWomen 2018
Kwenye maongezi ambayo yanapishana kwa kusikitisha na kuchekesha, mwandishi na mwanapodikasti Nora Mclnerny anashirikisha busara yake iliyopatikana kwa shida kuhusu maisha na kifo. Mtazamo wake wa wazi kwenye kitu ambacho, kwa kweli, kitatuathiri wote, ambacho ni huru na ni kigumu. Kwa nguvu zaidi, anatusisitizia kubadili jinsi tunavyoona maombolezo. "Mtu anaeomboleza ataenda kucheka na kutabasamu tena," anasema. "Wataenda kusonga mbele. Lakini haimaanishi wameendelea mbele."
TEDxAarhus
Bakteria "wanaongea" pamoja, wakituma taarifa za kemikali kuunda mashambulizi. Je kama tungesikiliza wanachosema? Mnanofizikia Fatima AlZahra's Alatraktchi ameunda kifaa cha kupeleleza mazungumzo ya bakteria na kutafsiri mazungumzo yao ya siri kwenda lugha ya binadamu. Kazi yake inaweza kuandaa njia ya ugunduzi wa mapema wa ugonjwa -- kabla hata hatujaumwa.
TED Residency
Marekani, kipimo cha damu cha kimoja, kinaweza kugharimu $19 katika kliniki moja na $522 katika kliniki nyingine majengo machache baadaye -- na hakuna ajuaye tofauti mpaka baada ya wiki moja wanapopata bili. Mwanahabari Jeanne Pinder anasema haihitaji kuwa hivi. Alijenga jukwaa ambalo linakusanya taarifa za gharama halisi za huduma za afya na kuweka taarifa wazi kwa wote, likifichua siri za bei za huduma za afya. Jifunze jinsi kujua gharama za vitu mapema kunavyoweza kutufanya tuwe na afya zaidi, na kuokoa pesa -- na kusaidia kurekebisha mfumo mbovu.
TEDWomen 2018
Duniani kote, wasichana weusi wanafukuzwa mashuleni kwa sababu ya sera ambazo zinalenga kuwapa adhabu, anasema mtunzi na mwanafunzi wa haki za jamii Monique W. Morris. Matokeo: wasichana wengi wanalazimika kuishia katika maisha yasiyo salama na yaliyo na fursa finyu za kufanikiwa kimaisha. Tunawezaje kuzuia janga hili? Katika hotuba yake yenye kuvuta hisia, Morris anafunua sababu za "kufukuzwa" na anaonyesha namna gani tunaweza kufanya shule kuwa sehemu ambazo wasichana wanaweza kupona na kufanikiwa.
TED@Merck KGaA, Darmstadt, Germany
Magari ya umeme yapo kimya sana, huleta ukimya mzuri katika majiji yetu. Lakini pia huleta hatari mpya, kutokana na kwamba yanaweza kumgonga kirahisi mtembea kwa miguu. Sauti gani yanatakiwa kutoa ili kufanya watembeaji kuwa salama? Pata maelezo ya namna gani sauti ya kesho itavyokuwa pale mhandisi wa sauti na mwanamuziki Renzo Vitale akionyesha namna anavyotengeneza sauti kwa ajili ya gari za umeme.
TED Salon Verizon
"Wapi panauma?" Ni swali ambalo mawanaharakati na mkalimu Ruby Sales alisafiri Marekani akiuliza, akiangalia kwa kina kwenye urithi wa nchi wa ubaguzi wa rangi na kutafuta vyanzo vya matibabu. Kwenye haya maongezi ya kuhamasisha, anashirikisha alichojifunza, akitafakari kwenye mda wake kama mpigania uhuru kwenye maandamano ya haki za kiraia na kutoa mawazo mapya kwenye njia ya haki za kitaifa.
TEDWomen 2018
Kwenye mazungumzo yenye nguvu, mkalimu Eldra Jackson III anatushirikisha jinsi alivyotelekeza mafunzo hatarishi kuhusu uwanaume kupitia Duara la Ndani, shirika linaloongoza tiba ya kikundi kwa wanaume waliokizuizini. Sasa anasaidia wengine kupona kwa kujenga taswira mpya ya kinachomaanisha kua mwanaume kamili na mzima. "Changamoto ni kutokomeza huu mzunguko wa ujinga wa hisia na mawazokundi," anasema.
TED Salon Brightline Initiative
Unataka kujifunza lugha mpya lakini unaogopa au hauna uhakika wapi pa kuanzia? Hauhitaji kipaji chochote maalumu au "jeni ya lugha," anasema Lýdia Machová. Katika hotuba hii changamfu, yenye hamasa, anaeleza siri za wanaisimu(watu wanaoongea lugha nyingi) na anashirikisha kanuni nne za kusaidia kufungua kipaji chako kilichojificha cha lugha -- na kufurahia wakati ukifanya hivyo.
TED@BCG Toronto
Unaangalia kwa ukaribu? Mfundishaji wa uono Amy Herman anaelezea namna ya kutumia sanaa kuongeza uwezo wako mtazamo na kupata muunganisho pale ambapo hauonekani kwa kawaida. Jifunze namna ambazo Herman anatumia kufundisha wanamaji wa SEAL, matabibu na wapelelezi wa uhalifu kubadili taarifa katika maarifa ya matendo kwenye hotuba hii yenye maelezo ya kina.
TED Salon Brightline Initiative
Mwandishi AJ Jakobs alianzisha safari na wazo linaloonekana rahisi kutoka moyoni: kushukuru binafsi kila mtu aliesaidia utengenezaji wa kikombe chake cha asubuhi cha kahawa. Zaidi ya "asante" elfu moja baadae, Jakobs anakumbukia safari yake ya kishindo duniani iliotokea -- na kushirikisha hekima ya kubadili maisha aliopata njiani. "Niligundua kua kahawa yangu isingekuwepo bila ma mia ya watu ninaowachukulia poa," Jakobs alisema.
TEDxCambridge
Namna gani tunaweza wafanya watu kutenda mema: kwenda kwenye uchaguzi, kutoa misaada, kutumia rasilimali au kwa ujumla kuwa wastaarabu kwa wengine? Mtafiti na mwanasayansi wa MIT anashirikisha listi ndogo ya mambo ya kufanya ya namna ya kupata nguvu ya sifa -- tamaa yetu kama binadamu kuonekana kama wastaarabu na wema badala ya wabinafsi -- kuhamasisha watu kufanya vitu kwa manufaa ya wengine. Jifunze zaidi kuhusu namna ambavyo mabadiliko madogo katika mikakati yako ya kuwafanya watu kufanya mema na pia kupata matokeo bora ya kushangaza.
We the Future
Kipokea barua pepe cha Ozlem Cekic kimejaa barua za chuki tangu 2007, aliposhinda kiti kwenye bunge la Denmark -- akiwa mmoja wa wanawake Waislamu kufanya hivyo. Mwanzoni alikua akifuta tu hizo barua, na kuziondoa kama kazi ya mashabiki, mpaka siku moja rafiki yake alivyotoa wazo lisilotarajiwa: awafikie waandishi wa hizo barua za chuki na kuwakaribisha wakutane kwa kahawa. Mikutano mia ya "mazungumzo kahawa" baadae, Cekic alishirikisha jinsi mazungumzo ya uso-kwa-uso yanaweza kua moja ya misukumo yenye nguvu kudhibiti chuki -- na inatupa changamoto sisi sote kushirikiana na watu tusiokubaliana nao.
TED Salon Verizon
Mbunifu wa teknolojia Fadi Chehade alitusaidia kuweka miundombinu inayotengeneza kazi ya intaneti -- vitu muhimu kama mfumo wa jina la kikoa na viwango vya anuani za IP. Leo amelenga kutafuta njia za jamii kufaidi kutoka kwenye teknolojia. Kwenye mazungumzo ya kuchechemua na Bryn Freedman, msimamizi wa taasisi ya TED, Chehade alijadili vita vinavyoendelea kati ya Magharibi na China juu ya ufahamu bandia, jinsi makampuni ya teknolojia yanaweza kuwa makarani wa nguvu walizonazo kuunda maisha na uchumi na nini wananchi wa kila siku wanaweza kufanya kudai nguvu juu ya intaneti.
TED@UPS
Huwa unaagiza nguo mtandaoni katika ukubwa na rangi mbalimbali, ili tu kujaribisha na kisha kurudisha ambazo hazikufai? Aparna Mehta alikuwa akifanya hivi nyakati zote, mpaka ilipofika siku alipojiuliza: Ni wapi ambapo nguo zinazorudishwa huenda? Katika hotuba yake ambayo inafumbua macho, anatufunulia dunia isiyoonekana ya "mrejesho wa bure wa bidhaa za mtandaoni" -- ambapo, badala ya kurudi katika makabati, hupelekwa katika jalala takribani paundi bilioni kila mwaka -- na anatueleza mpango wa kusaidia kukomesha ukuaji wa janga hili la kimazingira.
TED2018
Chanjo ya malaria ilibuniwa zaidi ya karne iliyopita -- ila kila mwaka, mamia na maelfu ya watu bado wanakufa na ugonjwa huo. Tutawezaje kuboresha chanjo hii muhimu? Kwenye haya maongezi ya kujulisha, mkingamaradhi na jamaa wa TED Faith Osier aonyesha jinsi anachanganya teknolojia ya kisasa na fahamu za ukubwa wa karne kwa matumaini ya kujenga chanjo mpya itakayotokomeza malaria kabisa.
TED2018
Itakuaje kama tutaweza saidia miili yetu kupona haraka bila makovu, kama Wolverine kwenye X-Men? Mshiriki wa TED Kaitlyn Sadtler anafanya kazi ili ndoto hii iwe kweli kwa kutengeneza vifaa vya biolojia vipya vinavyoweza kubadili jinsi mfumo wetu wa kinga unavyojibu majeraha. Kwenye mazungumzo haya mafupi, anaonyesha njia tofauti ambazo bidhaa hizi zinaweza kusaidia mwili ukajijenga upya.
TEDGlobal 2017
Sehemu iitwayo Agbogbloshie, jamii iliyopo Accra, Ghana, watu huenda kwenye jalala kuokota vifaa vibovu vya kielectroniki ili kupata malighafi. Bila mafunzo maalumu, wachimbaji hawa wa mjini hujifunza wenyewe jinsi gani vifaa hivi vinafanya kazi kwa kuvifungua na kuvifunga tena. Mshiriki wa TED DK Osseo-Asare anajiuliza: Kipi kitatokea kama tutaunganisha mafundi hawa waliojifundisha pamoja na wanafunzi na vijana wataalamu katika nyanja ya STEM(Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati)? Matokeo: jamii ya waundaji iliyo kubwa ambapo watu wanaungana pamoja na kuhamasika kutokana na kile wanachotaka kutengeneza. Jifunze zaidi ni namna gani sehemu hii ya uundaji inaongoza katika uchumi ulio na mzunguko katika ngazi ya chini.
TEDxSydney
Tumbaku inasababisha zaidi ya vifo milioni saba kila mwaka-- na baadhi yetu tunahusishwa na tatizo hili kadri ya tunavyodhani. Katika mazungumzo ya wazi, Dr. Bronwyn Kingi asimulia jinsi alivyogundua kwa undani, uhusiano kati ya sekta ya tumbaku na sekta ya fedha ulimwenguni inayoekeza fedha zetu kupitia mabenki makubwa, bima na malipo ya uzeeni. Jifunze vile Dr. King amesisimua msuko kuunda uwekezaji usiotegemea tumbaku na jinsi tunaweza saidia kumaliza janga hili.
TEDNYC
Wanamuziki wawili Anielle Reid na Matthew Brookshire (wakicheza pamoja kama Boy Girl Banjo) wamechukua jukwaa la TED kuimba wimbo wao waliotunga "Dead Romance" yaani "Mapenzi Yaliyokufa", wakisuka pamoja sauti za muziki wa asili ya Kimarekana na muziki wa kisasa wa pop.
TED2018
Trakoma ni ugonjwa wa macho wenye maumivu ambao husababisha upofu. Umekuwepo kwa takribani maelfu ya miaka, na karibuni watu milioni 200 duniani wapo katika hatari ya ugonjwa huu. Kinachoudhi ni kwamba, anasema Caroline Harper, unaweza kutibika kabisa. Akiwa na taarifa za kutosha kutoka mradi wa ramani ya sehemu zenye trakoma, taasisi yake ya Sightsavers wana mpango: kuweka juhudi katika nchi ambazo zina fedha za kuondoa tatizo -- na kuweka mkazo wa juhudi zaidi pia katika nchi ambazo zina mahitaji makubwa. Lengo: kuufanya ugonjwa ubaki kuwa historia katika vitabu tu. Mradi huu imara ni moja ya mawazo ya Audacious Project, mpango mpya wa TED wa kuhamasisha mabadiliko ya kiulimwengu.
TED2018
Katika mdahalo unaoendelea juu ya wakimbizi, tunasikia kutoka kwa kila mtu --- kutoka kwa wanasiasa ambao wanaahidi udhibiti wa mipaka kwa wananchi wanaoogopa kupoteza kazi zao -- kila mmoja, yaani, isipokuwa wahamiaji wenyewe. Kwa nini wanakuja? Mwanahabari na Mshiriki wa TED Yasin Kakande anaelezea nini kilochomsukuma yeye na wengine wengi kukimbia nchi zao, akisisitiza majadiliano ya wazi zaidi na mtazamo mpya. Kwa sababu simulizi la ubinadamu, anatukumbusha, ni simulizi la uhamaji: "Hakuna vikwazo ambavyo vingeweza kuwa madhubuti sana kuzuia wimbi la uhamaji ambalo limeamua historia yetu ya binadamu," anasema.
TEDGlobal 2017
MwanaTED Nighat Dad anasomea unyanyasaji wa mtandao, hasa inavyolingana na utamaduni kama ule wa kijiji chake cha Pakistani. Anahadithia vile alivyoanzisha laini ya kwanza ya msaada wa kwanza wa Pakistani wa unyanyasaji wa mtandao, unaowasaidia wanawake wanaokabiliana na ukandazamizaji katika mtandao, "Utumizi salama wa mtandao ndipo ujuzi unapopatikana, na ujuzi ni haki," anasema.
TED Residency
Malika Whitley ni mwanzilishi wa ChopArt, shirika kwa ajili ya vijana wadogo wasio na makazi ambalo limejikita katika ushauri, heshima na fursa kupitia sanaa. Katika simulizi hili binafsi na lenye hamasa, anashirikisha kisa chake cha kukosa makazi na kupata sauti yake mwenyewe kupitia sanaa -- na wito wake kutoa nafasi ya kibunifu kwa wengine ambao wamesukumizwa pembezoni mwa jamii.
TEDGlobal 2017
Nini tunachojua hasa kuhusu mbu? Fredros Okumu anakamata na kujifunza hawa wadudu wabeba-ugonjwa kama kazi -- na tumaini la kuponda makazi yao. Jiunge na Okumu kwenye matembezi ya mstari wa mbele ya tafiti za mbu, akieleza kiundani baadhi ya njia zisizo za kawaida ambazo timu yake ya Taasisi ya Afya Ifakara ilioko Tanzania imeendeleza kulenga kilichoelezewa kama mnyama hatari zaidi duniani.
TEDGlobal 2017
Peter Ouko alitumikia miaka 18 katika jela ya Kamiti, muda mwingine alikuwa akifungwa katika chumba cha jela na watu wazima 13 kwa masaa 23 na nusu kwa siku. Katika hotuba hii endelevu, anaelezea hadithi ya namna gani alivyokuwa huru -- na misheni ya mradi wa jela zilizopo Afrika: kuweka shule ya kwanza ya sheria iliyopo jela na kuhamasisha watu waliopo jela kuleta mabadiliko chanya.